Dodoma FM

Mikataba ya watumishi wa ndani kusaidia kupatikana kwa haki zao

14 August 2026, 16:51

Uelewa wa wananchi juu ya mikataba ya watumishi wa ndani inasaidia mtumishi kupata haki zake. Picha na Mtandao.

Watumishi wa ndani wanaokumbana na unyanyasaji wametakiwa kutambua kuwa vitendo hivyo si sehemu ya kazi, kuhifadhi ushahidi wa unyanyasaji na kutoa taarifa kwa mwajiri au mtu anayeaminika, pamoja na kutafuta msaada kutoka mamlaka na taasisi zinazohusika na masuala ya ajira na unyanyasaji.

Na Daniel Njau.

Waajiri wametakiwa kuhakikisha wafanyakazi wa ndani wanapewa mikataba ya ajira na kulipwa stahiki zao kwa mujibu wa makubaliano, baadhi yao wamekuwa wakikabiliwa na ucheleweshaji wa mishahara au kutolipwa kabisa.

Baadhi ya wananchi wamesema mkataba wa ajira ni haki ya kila mfanyakazi na unapaswa kuzingatiwa na pande zote mbili, huku wakisisitiza kuwa wafanyakazi wa ndani wanapaswa kuheshimiwa na kutambuliwa kama wafanyakazi wengine katika jamii.

Kwa upande wake mwanasheria Hope Katabwa amesema waajiri  wanatakiwa kufahamu kuwa mkataba wa ajira unapaswa kusainiwa na mtu mwenye umri wa miaka 18 au zaidi na mwenye uwezo wa kufanya maamuzi, lakini changamoto kubwa imeelezwa kuwa ni ukosefu wa elimu kwa baadhi ya wafanyakazi wa ndani kuhusu haki na wajibu wao unaotokana na mikataba hiyo.

Sauti na Daniel Njau.