Dodoma FM

Serikali yawekeza bil 67.9 kuboresha miundombinu ya TIA

7 September 2026, 16:26

Prof.William Palangio, amesema uwekezaji huo umewezesha kuboresha miundombinu katika kampasi za Mbeya, Mtwara,Singida, Mwanza pamoja na Zanzibar. Picha na Anwary Shabani.

Uwekezaji huo unaendelea kuonesha jitihada za Serikali katika kuimarisha miundombinu ya elimu ya juu na kuhakikisha taasisi za elimu zinakuwa na mazingira bora ya kutoa mafunzo yenye kukidhi mahitaji ya soko la ajira na maendeleo ya Taifa.

Na Anwary Shabani.  

Serikali imewekeza shilingi bilioni 67.9 katika kipindi cha miaka mitano, kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania — TIA, hatua inayolenga kuimarisha mazingira ya utoaji wa elimu na kuongeza ufanisi wa taasisi hiyo.

Akizungumza katika Idara ya Habari Maelezo jijini Dodoma, Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Profesa William Amos Palangio, amesema uwekezaji huo umewezesha kuboresha miundombinu katika kampasi za Mbeya, Mtwara, Singida, Mwanza pamoja na Zanzibar.

Profesa Palangio amesema mbali na uwekezaji huo, kupitia mradi wa HIT, Taasisi ya Uhasibu Tanzania imepokea jumla ya shilingi bilioni 27.8, fedha ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa miradi mbalimbali, ikiwemo mradi wa Singida ambao kwa sasa umefikia asilimia 72 ya utekelezaji.

Aidha, amesema mradi huo wa HIT unaotekelezwa Singida umekuwa na manufaa kwa wananchi, ambapo jumla ya Watanzania 275 wamepata fursa mbalimbali kupitia mradi huo, ikiwemo ajira.

Sauti na Anwary Shabani.