Dodoma FM
Dodoma FM
27 April 2026, 15:17

Amesema wamefikia hatua hiyo kutokana na ugonjwa wa nguruwe unaosababishwa na virusi na hauna tiba wala kinga .
Na Steven Noel.
Kaimu Afisa Mifugo Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Dkt. Emanuel Lyimo amesema kufuatia kuwepo wa ugonjwa wa nguruwe kwa baadhi ya maeneo katika wilaya ya Mpwapwa wamepiga marufuku kuingiza au kusafirisha nyama, mnyama au aina yoyote ya bidhaa zitokanazo na mnyama huyo kwa lengo la kudhibiti ugonjwa.
Dkt Lyimo amesema wakulima wengi wamepata hasara kutokana na wanyama wao kufa.
Wakiongea na Taswira ya Habari, baadhi ya wananchi wilayani Mpwapwa wameiomba serikali kufanya utafiti ili kuzuia ugonjwa huo kwani unapelekea wafugaji kupata hasara.