Dodoma FM

Vijana watakiwa kujiunga na mfumo wa NeST ili kunufaika na tenda za serikali

25 May 2026, 17:01

Ni vema Serikali kuendelea kutoa elimu juu ya mfumo huo ambao unaweza kuwa na tija.Picha na mtandao.

Mfumo wa Ununuzi wa Kielektroniki (NeST) ni fursa mahususi inayowawezesha vijana kupata zabuni za serikali kwa urahisi kwani Kupitia mfumo huu, serikali imetenga asilimia ya tenda maalum kwa ajili ya vijana, wanawake, wazee, na watu wenye ulemavu bila kushindana na makampuni makubwa.

Na Victor Chigwada.

Vijana wanao jishughulisha na ufundi wa sekta mbalimbali wametakiwa kuunda vikundi Kisha kujiunga kwenye mfumo wa kitaifa wa ununuzi wa kielektronik(Nest) Ili kunufaika na tenda za Serikali zinazo tolewa kupitia mfumo huo.

Hayo yamebainishwa na Afisa maendeleo wa Kata ya Ihumwa Bi.Anna Masijita ambapo amesema kumekuwa na tenda nyingi zinazo tangazwa na Serikali kupitia mfumo wa NeST ambazo zinalenga kuwapa tenda makundi mbalimbali ya vijana na wanawake

Sauti ya Bi.Anna Masijita.

Masijita amesema kuwa kupitia mfumo huo kwasasa hakuna tenda za kwenda kuomba ofisini ama katika Halmashauri hivyo njia Bora nikutengeneza vikundi na kujiunga katika mfumo wa NeST.

Sauti ya Bi.Anna Masijita

Nao baadhi ya vijana wamesema kuwa ni vema Serikali kuendelea kutoa elimu juu ya mfumo huo ambao unaweza kuwa na tija Kwa vikundi mbalimbali vya vijana.

Sauti za Vijana.