Dodoma FM

Wazazi wahimizwa kuzingatia ratiba ya chanjo kwa watoto

13 August 2026, 17:34

Wazazi watakiwa kuwapeleka watoto kupata chanjo kwa wakati ili kuwalinda watoto dhidi ya magonjwa. Picha na mtandao.

Wazazi na walezi wanahimizwa kupata taarifa sahihi kutoka kwa wataalamu wa afya na kuhakikisha watoto wanapata chanjo kwa wakati kulingana na ratiba waliyopewa.

Na Elizabeth.

Wazazi na walezi wametakiwa kuzingatia chanjo za awali kwa mtoto ili kumkinga mtoto na magonjwa mbalimbali.

Licha ya chanjo kuwa miongoni mwa huduma muhimu za kinga kwa watoto, baadhi ya wazazi na walezi bado hukabiliwa na changamoto zinazowafanya kuchelewa au kutowapeleka watoto kupata chanjo kwa wakati.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wananchi ambao wameeleza uelewa wao juu ya umuhimu wa chanjo kwa watoto huku wakitaja baadhi ya changamoto zinazo wakamisha kuwapeleka watoto wao kupata chanjo kwa wakati.

Kwa upande wake mkunga na mtaalamu wa afya ya mama na mtoto Midwife Anitha Mganga amesema  ni muhimu wazazi na walezi kupata taarifa sahihi kuhusu ratiba ya chanjo, huku jamii ikihimizwa kushirikiana na wahudumu wa afya katika kuhakikisha watoto wanapata chanjo kwa wakati.

Sauti na Elizabeth.