Wananchi watakiwa kuzingatia usafi binafsi ili kuepuka magonjwa
4 September 2026, 16:20

Kemilembe dominick ni mtaalamu wa afya mwanafunzi yeye anasema mtu anapaswa kuwa na utaratibu wa kuoga na kusafisha mwili, kutunza meno, kucha na nywele, pamoja na kunawa mikono kwa sabuni. Anaongeza kuwa usafi wa mwili unapo zingatiwa husaidia kupunguza hatari ya maambukizi na huongeza hali ya kujiamini.
Na Crispine Gerald.
Inaelezwa kuwa usafi wa mwili ni sehemu muhimu ya afya na ustawi wa mtu, Unao husisha kuoga na kusafisha mwili, kunawa mikono, kutunza meno, nywele na kucha, pamoja na kuvaa nguo safi.
Usafi binafsi ni muhimu katika kuzuia kuenea kwa magonjwa na kulinda afya kwa mujibu wa shirika la afya Duniani (WHO) linapendekeza watu kunawa mikono kwa sabuni mara kwa mara, hususan baada ya kutumia choo na kabla ya kula au kuandaa chakula.
Wananchi wanaeleza hatua wanazozingatia katika kutunza usafi wa miili yao kila siku, ikiwemo kuoga, kunawa mikono na kusafisha meno.