Serikali yaombwa kufanya tathmini uchakavu wa shule ya msingi Ikombolinga
16 July 2026, 12:23

Amesema licha ya kupokea fedha za mfuko wa Jimbo kwaajili ya ukarabati wa shule hiyo bado pesa hizo hazikidhi mahitaji ya ukarabati wa shule hiyo.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa kijiji cha Ikombolinga Wilayani Chamwino wameiomba Serikali kufanya tathimini ya hali ya uchakavu wa vyumba vya madarasa na majengo katika shule ya msingi Ikimbolinga kwani inahatarisha usalama wa wanafunzi.
Wakiongea na taswira ya habari wakazi wa kijiji hicho wamesema uchakavu wa majengo na fenicha shuleni hapo unapelekea watoto kuogopa kuhudhuria masomo kila siku hivyo wanaiomba serikali kuikumbuka shule hiyo na kuifanyia ukarabati.
Taswira ya habari imezungumza na mwenyekiti wa maendeleo Kata ya Ikombolinga Bw. Mtemi Matonya ambapo amesema ni kweli shule hiyo imekuwa ni chakavu kwenye majengo kutokana na ujenzi wake kuwa wa muda mrefu
Amesema licha ya kupokea fedha za mfuko wa Jimbo kwaajili ya ukarabati wa shule hiyo bado pesa hizo hazikidhi mahitaji ya ukarabati wa shule hiyo.