Mlebe waipongeza serikali kwa kuwasogezea huduma ya maji
5 June 2026, 16:54

kwa sasa wananchi wa eneo hilo wanapata maji kwa urahisi tofauti na awali.
Victor Chigwada.
Wakazi wa kitongoji cha Nyerere kijiji cha Mlebe wameipongeza Serikali Kwa kushirikiana na shirika la innovation of Africa Kwa kuwasogezea karibu huduma ya maji safi na salama .
Wakieleza kufurahishwa kwao na mradi huo wa maji wananchi hao wamesema imekuwa nafuu kwao kwani kwasasa wako huru na majukumu mengine tofauti na hapo awali ambapo iliwalazimu kutumia muda mrefu kutafuta maji na kushindwa kufanya shughuli zingine.
Taswira ya habari imeongea na mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Joseph Mpilini ambapo amesema kwa sasa wananchi wa eneo hilo wanapata maji kwa urahisi tofauti na awali wakati mradi huo haujafika kijijini hapo