Dodoma FM

Wazazi, walezi watakiwa kutowaficha watoto wenye ulemavu

31 July 2023, 6:33 pm

Mkuu wa wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Mhe. Abdallah Mwaipaya akizungumza walipotembelea shule ya Mwanga Viziwi. Picha na ofisi ya Waziri Mkuu.

Jamii imeendelea kusisitizwa kutowaficha watoto wenye changamoto ya ulemavu wowote bali iwaweke wazi ili waweze kupatiwa mahitaji ya msingi ikiwemo elimu.

Na Pius Jayunga.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amewataka wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu kutowaficha watoto wao ndani akisema kufanya hivyo ni kuwanyima haki zao za msingi.

Mhe. Ummy ametoa kauli hiyo katika ziara yake alipotembelea wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwanga Viziwi, wilaya ya Same pamoja na wilaya ya Mwanga  mkoani  Kilimanjaro  kwa lengo la kufuatilia  utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Amesema kuwa watu wenye ulemavu wana haki sawa na watu wengine hivyo inapaswa kushirikishwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi pamoja na fursa ili waweze kujikwamua kiuchumi na kutoa mchango wao katika maendeleo ya Taifa.

Sauti ya Mhe. Ummy Nderiananga
Picha ni Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA), wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Bwa. Jeremia Shayo. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Naye mkuu wa wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Mhe. Abdallah Mwaipaya ameishukuru serikali kwa kuanzisha shule za watu wenye ulemavu kwani hutoa fursa kwao kupata ujuzi na stadi za maisha.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro

Akitoa taarifa ya watu wenye ulemavu katibu wa Shirikisho la Vya vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA), wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Bwn. Jeremia Shayo ameeleza kwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa viungo bandia pamoja na wakalimani wa lugha ya alama katika baadhi ya taasisi hivyo kukwamisha mawasiliano.

Sauti ya Katibu wa SHIVYAWATA wilaya ya Mwanga