Dodoma FM

Afisa elimu Msingi Bahi atoa Motisha kwa walimu kata ya Bahi

28 April 2023, 12:23 pm

Picha Afisa Elimu Msingi wilaya ya Bahi alipofika kutoa motisha shule ya Msingi Bahi sokoni. Picha na Bernad Magawa.

Afisa Elimu katika kata hiyo ameahidi kuhakikisha ufaulu unapanda zaidi.

Na Bernad Magawa.

Afisa elimu Msingi wilaya ya Bahi Boniface Wilson ametoa motisha ya kilo 25 za sukari kwa kila shule kwenye kata ya Bahi yenye jumla ya shule tano za msingi kama motisha baada ya kata hiyo kufaulisha wanafunzi wote wa darasa la saba mwaka 2022 na kushika nafasi ya kwanza katika wilaya hiyo

Wilson amesema ameamua kutoa motisha hiyo ili kuongeza ari ya kazi kwa walimu kutokana na juhudi zao kubwa katika ufundishaji.

Sauti ya Afisa elimu Msingi wilaya ya Bahi Boniface Wilson
Afisa Elimu Msingi wilaya ya Bahi akizungumza na wanafunzi alipofika kutoa motisha shule ya Msingi Bahi sokoni. Picha na Bernad Magawa.

Akizungumza kwa niaba ya walimu wa kata hiyo, Afisa elimu kata ya Bahi Dansent Kyamba amemshukuru kiongozi huyo kwa kujali juhudi za walimu wake huku Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Bahi sokoni John Josephat akiahidi kuhakikisha ufaulu unapanda zaidi kwa mwaka huu.

Sauti ya Afisa elimu kata ya Bahi Dansent Kyamba .