Dodoma FM

Simulizi ya makaburi ya wahanga katika eneo la Mathius Kata ya Miyuji Dodoma

27 March 2023, 3:41 pm

Eneo la makaburii ya wahanga wa treni katika mtaa wa Mathius jijini Dodoma.Picha na Martha Mgaya

Hii hapa simulizi nzima ya ajali ya treni hiyo na ni kwanini eneo hilo limeitwa eneo la makaburi ya wahanga.

Na Martha Mgaya.

Tarehe 24 juni 2002 ni tarehe isiyo sahaulika katika kumbukumbu ya wana Dodoma na watanzania wote kwasababu ya ajali ya treni iliyotokea kati ya stesheni ya Msagali na Igunga Dodoma na hili likiwa eneo la Makaburi ya 88 kati ya 288 ya wahanga wa ajali hiyo waliozikwa juni 27 siku tatu tu baada ya ajali kutokea.

Na hapa tukiendelea kuelezewa simulizi hiyo na tukumbuke historia ya mzee Mathius ambayo eneo hili lilikuwa ni eneo la mzee huyo na alilitoa kwaajili ya maziko na baada ya kutokea kwa ajali ya treni basi alilitoa kwaajili ya wahanga wa ajali hiyo kuzikwa hapo.