Dodoma FM

Wakazi wa Dodoma watakiwa kuzingatia elimu ya kisiki hai.

19 August 2021, 1:06 pm

Na;Yussuph Hans.

Wakulima na wafugaji Mkoani Dodoma wameshauriwa kuzingatia elimu ya kisiki hai itakayowasaidia kuwa na kilimo bora pamoja na malisho ya kutosha kwa wanyama.

Ushauri huo umetolewa na Mratibu wa Mradi wa kisiki hai Wilaya ya mpwapwa Olipa chipwaza wakati akizungumza na taswira ya habari ambapo amesema kuwa kuwa njia ya kisiki hai inaweza kurudisha miti kwa haraka mashambani na katika sehemu za malisho.

Ameongeza kuwa kwa wakulima katika mikoa yenye ardhi kame njia ya kisiki hai inasaidia zaidi kuwahakikishia wafugaji chakula cha uhakika kwa mifugo yao.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wafugaji mkoani hapa wamekiri kuapata changamoto katika kipindi cha kiangazi huku wakisema kuwa suala la utunzaji wa mazingira ni muhimu katika kupata malisho ya kutosha.

Kisiki Hai ni njia ya kutunza maotea ya miti yanayochipua kutokana na Kisiki Hai au Mbegu za miti zilizodondoshwa ardhini na vinyesi vya wanyama au ndege.