Dodoma FM

Ujenzi daraja la Munguri kuanza Januari mwakani

4 December 2023, 4:45 pm

Picha ni Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa akizungumzia ujenzi wa daraja hilo la Munguri wilayani Kondoa. Picha na Nizar Mafita.

Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amesema daraja hilo ni lazima lijengwe kwa kuwa ni daraja la kitaifa.

Na Nizar Mafita.

Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amethibitisha  ujenzi wa daraja la Munguri kuanzia mwezi Januari mwakani.

Akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Bashungwa, Diwani wa kata ya Serya Kulwa Pazia amesema wananchi wa kata hiyo pamoja na kata jirani wamekuwa na adha kubwa ya kushindwa kuvuka katika mto huo pindi wanapotafuta matibabu na mahitaji mengine Kondoa mjini

Sauti ya Bw. Kulwa Pazia.

Nao wabunge wa Kondoa Ally Makoa na Ashatu Kijaji wamesema kutokwepo kwa daraja hilo la Munguri linachangia kuzorotesha hali ya uchumi kwa wananchi kwa kuwa hufanya shughuli za kilimo na uvuvi wa samaki katika maeneo hayo.

Sauti za Ally Makoa na Ashatu Kijaji.

Waziri Bashungwa amethibitisha kuwa daraja Hilo ni la kitaifa hivyo ujenzi wake utanza Mwezi January 2024 baada ya usanifu wa kina kufanyika.

Sauti ya Mh. Innocent Bashungwa.