Dodoma FM

Chinugulu walalamika kukosa mikopo ya asilimia 10

27 April 2026, 12:59

Wananchi hao wamesema tangu kuanza kwa awamu nyingine ya mikopo ya halmashauri wamejitahidi kujiunga na vikundi na kuomba mikopo hiyo.Picha na Mtandao.

Juhudi za kumtafuta Afisa maendeleo kata ya Chinugulu kuzungumzia ishu ya wananchi kushindwa kupata mikopo licha ya vikundi walivyo anzisha bado zinaendelea .

Na Victor Chigwada.

Vijana wa kitongoji cha Kilimoni Siasa katika Kijiji cha Chinugulu Wilayani Chamwino wamehoji kama mikopo ya asilimia kumi inayafikia makundi yote yaliyo lengwa na serikali.

Hayo yanajiri baada ya vikundi vya kijiji cha Chinugulu vilivyo anzishwa ili kunufaika na mkopo huo havijapata mkopo hata mara moja.

Wakiongea na taswira ya habari wananchi hao wamesema tangu kuanza kwa awamu nyingine ya mikopo ya halmashauri wamejitahidi kujiunga na vikundi na kuomba mikopo hiyo lakini hawajafanikiwa kupata.

Sauti za wananchi.

Daniel Njelula Mwenyekiti wa Kijiji cha Chinugulu amekiri kuwa pamoja na mwitikio mkubwa wa wananchi kuanzisha makundi ili waweze kunufaika na mkopo huo lakini hawajapatiwa mkopo hadi sasa.

Sauti ya Daniel Njelula.