Dodoma FM

Wazazi wa kiume waomba kushirikishwa huduma hedhi salama

21 July 2026, 16:03

Endapo siri itaondoka katika familia kuhusu Hedhi Salama kwa mtoto wa kike itamsaidia binti kuwa na Afya ya Uzazi bora. Picha na mtandao.

Ameongeza kuwa ushirikiano wa wazazi wote ni muhimu ili kuhakikisha hakuna binti anayetoka shule kwa sababu ya Hedhi.

Na Stephen Noel.

Wazazi na walezi wa kike wametakiwa kuacha kuwaficha wazazi na walezi wa kiume katika suala la Hedhi Salama kwa watoto wa kike ili kushirikiana katika upatikanaji  wa malezi shirikishi  na vifaa saidizi pindi binti anapokuwa kwenye Hedhi.

Wito huo umetolewa na shirika la Marafiki Elimu wakati wakitoa Elimu ya Hedhi Salama kwa wanafunzi na wazazi wa Shule ya Sekondari Godegode iliyopo Wilaya ya Mpwapwa.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, mtoa Elimu kutoka Marafiki Elimu amesema endapo siri itaondoka katika familia kuhusu Hedhi Salama kwa mtoto wa kike itamsaidia binti kuwa na Afya ya Uzazi bora katika siku za usoni.

Mmoja wa wazazi wa kiume, Bw. Hadson Elias amekiri kuwa mara nyingi wazazi wa kike ndio huwaficha wazazi wa kiume katika suala la Hedhi na kusema ni wakati wa kubadilika.

Kwa upande wake Regina Afrikani, Mratibu wa Virabu vya Kupinga Ukatili Wilaya ya Mpwapwa amesema Elimu ya Hedhi tangu imeanza kutolewa imesaidia kupunguza unyanyapaa na kuwezesha mabinti kupata mahitaji yao kirahisi kutoka kwa wazazi wote wawili.

Sauti ya Noel.