Dodoma FM
26 August 2026, 17:13

Wananchi,wazazi, walezi na jamii kwa ujumla wametakiwa kutambua wajibu wao wa malezi, kuwaongoza watoto kwa nidhamu na kushirikiana na viongozi wa dini pamoja na jamii katika kujenga kizazi chenye maadili mema.
Na Daniel Njau.
Wananchi wameeleza kuwa mabadiliko ya maadili katika jamii ya nachangiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya wazazi na walezi kushindwa kutekeleza ipasavyo wajibu wao wa malezi.
Mshauri wa familia na malezi, Bw Dastan Haule, amesema wazazi wana nafasi kubwa katika kujenga tabia njema za watoto, akibainisha kuwa kuwapa watoto uhuru usio na mipaka na kushindwa kuwaonya wanapokosea kunaweza kuchangia kuporomoka kwa maadili.