Mgomo wa madereva wa kwamisha safari za mabasi Dodoma
29 September 2026, 16:38

Hatua hiyo imeibua mjadala kuhusu changamoto zinazo wakabili madereva wa mabasi ya masafa marefu, huku wadau wakitarajiwa kutafuta suluhisho litakalo wezesha huduma za usafiri kuendelea bila kuathiri usalama barabarani wala maslahi ya madereva.
Na Anwary Shabani.
Safari za mabasi ya mikoani zimekwama katika Kituo Kikuu cha Mabasi Nane nane jijini Dodoma, baada ya baadhi ya madereva kusitisha huduma hiyo wakipinga kile wanacho dai kuwa ni changamoto katika utekelezaji wa sheria na mazingira ya kazi.
Madereva hao wameeleza kuwa miongoni mwa sababu zilizo wasukuma kusitisha safari ni utekelezaji wa mfumo wa kukatwa pointi kwenye leseni za udereva , ambao wanadai unaathiri utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha, wamelalamikia namna ukaguzi na usimamizi wa magari unavyo fanyika barabarani , huku wakidai kukumbana na usumbufu kutoka kwa baadhi ya askari wa usalama barabarani wakati wakitekeleza majukumu yao.
Mbali na changamoto hizo , madereva hao pia wameeleza kutoridhishwa na mazingira ya ajira , wakidai kuwa wanapodai maslahi yao kutoka kwa waajiri, wakati mwingine hukumbana na hatua za kuondolewa kazini. Kutokana na hatua hiyo , wasafiri waliokuwa wakitarajia kusafiri kutoka Dodoma kwenda mikoa mbalimbali wamekumbwa na usumbufu wa usafiri, huku baadhi yao wakilazimika kusubiri kituo hicho