Dodoma FM

Waumini wa dini ya kiislamu wameomba msaada kukamilisha Madrasa

6 October 2026, 17:30

Pichani ujenzi wa madrasa umesimama kutokanan na ukosefu wa wafadhili. Picha na mtaa kwa mtaa blog.

Waumini wa dini ya Kiislamu katika Kijiji cha Mtakuja, Kitongoji cha Lusangi, Kata ya Dalai, Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, wameomba msaada wa wadau mbalimbali ili kukamilisha ujenzi wa madrasa yao.

Na Kitana Hamisi.

Waumini hao wamesema wamejitahidi kwa nguvu zao wenyewe kuendeleza ujenzi huo, lakini wamefikia hatua ambayo wanahitaji msaada wa fedha na vifaa vya ujenzi ili kukamilisha kazi iliyobaki.

Abduli Fatao, Msimamizi wa Madrasa, amesema juhudi za waumini zimewezesha ujenzi kufikia hatua iliyopo, lakini bado kuna mahitaji muhimu yanayohitaji msaada.

Mwalimu Juma Mtandala, Imamu, amewataka wadau na wananchi wenye uwezo kujitokeza kusaidia, akieleza kuwa kukamilika kwa madrasa hiyo kutatoa mazingira bora kwa watoto kupata elimu ya dini.

Naye Amina Salimu Ndongolo pamoja na Zaituni Saidi wameomba jamii na wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi zao ili madrasa hiyo ikamilike na kuanza kutumika kikamilifu.

Simulizi na Kitana Hamisi.