Dodoma FM
27 October 2026, 17:31

Baadhi ya vijana wametoa maoni yao juu ya mchezo wa kubashiri maarufu kama “ kubeti kuwa sio ajira kwani bila kianzio cha pesa huwezi kucheza ili ushinde.
Na Yassin Athuman.
Kwa mujibu wa gazeti la nipashe la hivi karibuni takribani asilimia 47 ya vijana wa Tanzania wanajihusisha na masuala ya mchezo wa kubeti au kubashiri, wakidai kuwa ni njia inayowapatia kipato kutokana na ukosefu wa ajira.
Adha, wamesema mtu kuamua kushiriki kwenye michezo ya kubashiri ni maamuzi yake mwenyewe huku wakiiomba serikali kuingilia kati kuwadhibiti vijana ambao wanashinda kwenye michezo hiyo kutwa nzima na kushindwa kufanya shughuli za maendeleo.