Dodoma FM

Kazi za ubunifu zinawezaje kumuongezea mwanamke kipato

16 November 2026, 17:03

Kwa kutumia teknolojia hizi, wanawake wanapata maarifa, mitandao na fursa za kuendeleza ubunifu wao kwa njia jumuishi.Picha na Agentz.

Pale watu unaofanya nao kazi wanaona mawazo yao ya kibunifu yanafanyiwa kazi itawapa hamasa zaidi ya kuzidi kuwa wabunifu zaidi na hii huchipua ufanisi katika kazi.

Kutokana na uchunguzi ulofanywa na jarida la Upreners wa mwaka 2018 umeonesha kua asilimia 68% ya watu wengi katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, hujihisi kuwa katika hali shinikizo [kutokuwa na utulivu wa kiakili na Amani] kiasi cha kutokuwa na ufanisi wala ubunifu katika kazi zao na kuishia kufanya kazi nyingi zisizo katika ubora tarajiwa.

Kuwa na mawazo ya kibunifu ni jambo jema lakini kuishia kuwa na mawazo ya kibunifu ni kazi bure, ni lazima kazi ya ziada ifanyike ya kutengeneza mazingira kwa ajili ya kuanza kufanyia kazi hayo mawazo ya kibunifu yaliyopatikana, unapokua umefanya uchunguzi yakinifu juu ya uwezekano wa kufanikiwa na kiutendaji wa wazo bunifu ni muhimu sana kuamua kuanza kuwekeza muda na rasirimali katika kuanza kulitendea kazi wazo hilo la kibunifu.