Dodoma FM

Kero ya uhaba wa madarasa yatatuliwa shule ya msingi Ihumwa

11 September 2026, 16:41

Kero ya madarasa Ihumwa imepata ufumbuzi wa madarasama mapya kwaajili ya wanafunzi kujisomea. Picha na mtandao.

Pamoja na kukamilika kwa shule hiyo, bado kuna matarajio ya kumalizia vyumba vya madarasa katika Kitongoji cha Ilolo pamoja na kujenga vyumba vingine katika Mtaa wa Chang’ombe.

Na Victor Chigwada.

Kero ya uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi Kata ya Ihumwa imeanza kupata ufumbuzi baada ya kukamilika kwa ujenzi wa vyumba 14 vya madarasa katika Mtaa wa Chilwana, ambavyo vinatarajiwa kuanza kutumika mwakani.

Mwenyekiti wa Maendeleo wa Kata ya Ihumwa, Edward Magawa, amesema licha ya kuwepo kwa shule mbili za Serikali, idadi kubwa ya watoto imekuwa tishio katika shule hizo, hali iliyowalazimu kuweka malengo ya kukabiliana na mlundikano wa wanafunzi katika chumba kimoja.

Magawa amesema hadi sasa kuna mafanikio baada ya kufanikiwa kujenga shule ya msingi yenye vyumba 14 vya madarasa katika Mtaa wa Chilwana, huku matumaini yakiwa ni kila shule kuwa na wastani wa wanafunzi 700 hadi 800.

Sauti na Victor Chigwada.