Wananchi Chamwino waomba elimu matumizi ya nishati mbadala
21 September 2026, 17:16

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mnase, Ayubu Malima, amesema kijiji hicho kinaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira, huku kikitekeleza kanuni ndogo ikiwemo kauli ya “kata mti, panda mti” pamoja na kuweka utaratibu wa kutoa vibali maalumu kwa shughuli zinazohusisha ukataji wa miti.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa vitongoji vya Sokoine na Malechela, katika Kijiji cha Mnase, Wilaya ya Chamwino, wameiomba Serikali kuwawezesha kupata nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi, hatua wanayosema itasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya kuni.
Wananchi hao wamesema upatikanaji wa gesi mbadala utawapa fursa ya kupunguza utegemezi wa kuni, ambazo hutokana na ukataji wa miti, huku pia ukisaidia kupunguza muda ambao wanawake hutumia kutafuta kuni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Wamesema ya nishati safi ya kupikia pia yanaweza kuwasaidia kupunguza matumizi athari za kiafya zinazoweza kuhusishwa na matumizi ya nishati zinazozalisha moshi mwingi, pamoja na kuchangia katika uhifadhi wa mazingira vijijini.