Tabia uzofanya unapo amka zinaweza kuwa mchango wa umakini wa siku nzima
26 August 2026, 17:06

Ameongeza kuwa ni muhimu mtu kuwa na uwezo wa kuendelea na majukumu yake hata pale ambapo hajafanya jambo alilozoea kufanya mara baada ya kuamka.
Je unafahamu kuwa tabia anazofanya mtu mara tu baada ya kuamka zinaweza kuwa na mchango katika umakini na msisimko wa mwili kwa shughuli anazotarajia kufanya siku hiyo.
Lakini wataalamu wa saikojia wanasema kuwa shughuli hizo si lazima ziwe na uwezo wa kuamua moja kwa moja hali yake ya kisaikolojia kwa siku nzima.
Haya yamesemwa na mwanasaikolojia na Mshauri Nasihi kutoka Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Peter Njau, amesema mambo anayofanya mtu baada ya kuamka kama kutumia simu, kufanya mazoezi au kula yanaweza kuathiri umakini na namna mwili unavyojiandaa kwa shughuli za siku.
Hata hivyo, Njau amesema hali inaweza kuwa tofauti pale mtu anapofikia hatua ya kutegemea jambo fulani kiasi kwamba asipolifanya hawezi kuendelea na shughuli zake, akieleza kuwa hali hiyo inaweza kuathiria utegemezi wa tabia hiyo.