

10 June 2025, 2:56 pm
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kijiji cha Mlebe hakuna vikundi vya vijana katika kijiji chake zaidi ya kikundi kimoja cha akina mama ambacho ndicho kipo hai mpaka sasa.
Na Victor Chigwada.
Vijana wa Kijiji cha Mlebe wametakiwa kuchangamkia fursa za mikopo ya Serikali kwani ndiyo yenye tija ya kuwakwamua kiuchumi Kwa kuendesha miradi mbalimbali ya kuwaingizia kipato
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Joseph Mpilimi ambacho kimeonekana vijana wanashindwa kuunda vikundi na kujikita katika shughuli mablimbali za uzalishaji
Mpilimi amesema kuwa ni wakati wa kuamka na kuzalisha na kuachana na kupoteza muda vijiweni bila kuzalisha Ile hali familia zinawategemea
Aidha ameongeza kuwa wapo ambao wamekuwa wakikopa kwenye mashirika binafsi ambayo baada ya muda yanageuka na kuwa mwiba kwao Kwa kushindwa kulipia riba ya mikopo hiyo
Tofauti na mikopo ya asilimia 10 ambayo unarudisha fedha uliyochukua pasipo na riba yoyote hivyo vijana wangeweza kunufaika zaidi na mikopo hiyo