Dodoma FM

Washiriki 100 wa uchumi challenge 2026 watangazwa

5 June 2026, 16:35

Picha ni Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya shindano hilo, Bi. Amina Sanga Akizungumza jijini Dodoma.Picha na Bennard Filbert.

Wakati huohuo, Serikali imeongeza zawadi za shindano hilo ambapo mshindi wa kwanza atapata shilingi milioni 50, wa pili milioni 30 na watatu milioni 20, huku washiriki wote 100 bora wakipata vyeti vya utambuzi na fursa za maendeleo ya kitaalamu.

Na Bennard Komba.

Serikali kupitia Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana imetangaza washiriki 100 bora walio fanikiwa kuingia hatua inayofuata ya Shindano la Vijana Uchumi Challenge 2026, baada ya kupokea maombi 7,852 kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza jijini Dodoma, Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya shindano hilo, Bi. Amina Sanga, amesema maombi 4,121 sawa na asilimia 52.5 yalikidhi vigezo, huku mawazo 458 yakifikia hatua ya mwisho ya uchambuzi kabla ya kupatikana kwa washiriki 100 bora.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, sekta ya TEHAMA na huduma za kidigitali imeongoza kwa asilimia 30.7 ya mawazo yaliyo wasilishwa, ikifuatiwa na Kilimo na Teknolojia za Kilimo kwa asilimia 27.8 na Viwanda pamoja na Uzalishaji kwa asilimia 21.3.

Washiriki walio chaguliwa watashiriki kambi maalum ya siku nne kwaajili ya mafunzo, kuboresha mawazo ya ona kujifunza mbinu za kufanya mawasilisho mbele ya majaji na wawekezaji.

Sauti ya Bi. Amina Sanga.