Dodoma FM

Wananchi Chang’ombe waiomba serikali kuboresha eneo la stendi

28 July 2026, 16:07

Picha ni baadhi ya wasafiri na mabasi yanayokwenda vijijini katika eneo hilo la Chang’ombe.Picha na Anwary Shaban.

Utekelezaji wa miradi hiyo unatarajiwa kuondoa changamoto za msongamano, kuongeza usalama wa watumiaji wa kituo hicho na kuboresha huduma za usafiri, sambamba na kukuza shughuli za kiuchumi katika eneo la Chang’ombe na Jiji la Dodoma kwa ujumla.

Na Anwary Shaban.

Wakazi wa kata ya Chang’ombe jijini Dodoma wameiomba serikali kuongeza ukubwa wa eneo la stendi na kuboresha miundombinu ya kituo hicho kwani kwasasa kituo hicho kipo katika mpangilio mbovu kutokana na udogo wa eneo.

Taswira ya habari ilizungumza na baadhi ya wananchi wa eneo hilo ambapo wamedai kuwa kituo hicho kinacho hudumia usafiri wa mabasi ya vijijini na daladala zinazo fanya mzungunguko wa kutoka Chang’ombe hadi mjini kipo katika eneo dogo hali inayo athiri shughuli za biashara katika eneo hilo.

Aidha wamesema msongamano wa magari katika eneo hilo unasababisha usumbumbu mkubwa hasa kwa wasafiri na wafanyabiashara hivyo wanaiomba serikali kupanua kituo hicho ili kuwapunguzia adha wanazo kutana nazo kila siku .

Kwa upande wake, Naibu Meya wa Jiji la Dodoma, Baraka Fundikira, ambaye pia ni diwani wa kata ya Chang’ombe amesema Halmashauri tayari imeanza mchakato wa kutekeleza miradi ya maendeleo katika Kata yaChang’ombe kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia.

Amesema miradi hiyo inajumuisha ukarabati wa Kituo cha Mabasi cha Chang’ombe pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, hatua zinazo lenga kuboresha huduma za usafiri na mazingira ya biashara kwa wananchi.

Sauti ya Anwary Shaban.