Jamii yaaswa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum kupata elimu
24 July 2026, 16:34

Wazazi na Wadau wasema unyanyapaa umepungua, mwamko wa kuwapeleka shule umeongezeka.
Na Stephen Noel
Jamii imeshauriwa kuendelea kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum ikiwemo kuwapatia haki ya kupata elimu.
Wakiongea na Dodoma FM baadhi ya wazazi wa watoto wenye mahitaji maalum na wadau wa Elimu wamesema kutokana na kuongezeka kwa uelewa kuhusu watoto wenye mahitaji maalum, mwamko wa jamii kuwapeleka watoto shule umeongezeka na unyanyapaa umepungua.
Mery Makunguru ni mzazi wa mtoto mwenye mahitaji maalum na Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Chazungwa anasema kutokana na uwekezaji wa Serikali na Elimu inayotolewa na wadau imeongeza hamasa ya wazazi kuwapeleka shule watoto wenye mahitaji maalum.
Shabani Mgwila ni Afisa Ustawi Wilaya ya Mpwapwa anasema Serikali itajitahidi kutekeleza afua na mikataba ambayo Serikali imeingia juu ya haki za watoto wenye mahitaji maalum.
Kwa upande wake Afisa kutoka Shirika la HakiElimu, Pius Makomelelo amesema kwa sasa mtoto wa kiume pia waanze kuzungumziwa katika majukwaa.