Dodoma FM

Shule shikizi Matomondo kuwaokoa wanafunzi kutembea km 7 kila siku

19 May 2026, 17:16

Picha ni jengo hilo la shule shikizi lililojengwa katika shule shikizi mbugani.Picha na Steven Noel.

Bado eneo hilo linakabiliwa na changamoto ya Wanafunzi wa shule ya sekondari matomondo kutembea umbali mrefu kila siku km 15 hadi shule ilipo.

Na Steven Noel.

Ujenzi wa shule shikizi katika kata ya Matomondo umesaidia kuondoa changamoto ya watoto wa darasa la kwanza kutembea umbali wa kilomita 7 kila siku kufuata shule ilipo.

Hayo yamesemwa na Diwani wa kata ya Matomondo Bw. Yoel Lechipya ambapo amesema kupatikana kwa madarasa hayo mawili katika shule shikizi mbugani kutawaepusha wanafunzi kutembea uumbali mrefu hali iliyokuwa inapelekea baadhi ya wanafunzi kuacha shule.

Bwana Lechipya amesema hayo alipokuwa akiongea na Taswira ya habari ambapo amesema baada ya kubaini changamoto hiyo serikali ilitoa fedha za kujenga majengo mawili Katika shule shikizi Mbugani na jengo Moja  Katika shule ya Msingi Tambi.

Aidha Bw Lechipya amesema bado eneo hilo linakabiliwa na changamoto ya Wanafunzi wa shule ya sekondari matomondo kutembea umbali mrefu kila siku km 15 hadi shule ilipo.

Kwa upande wake kaimu Afisa Elimu Mpwapwa bwana  Yohana Myovela amesema mfumo wa shule shikizi ni utaratibu wa utoaji wa Elimu kabla ya shule kusajiliwa.

Sauti ya kina