Dodoma FM

Unyonyeshaji wafikia asilimia 66 nchini

8 August 2025, 4:08 pm

Ni muhimu mtoto kupatiwa maziwa ya mama pindi anapozaliwa kwani maziwa hayo yana vrutubisho vyote muhimu kwa mtoto.Picha na Lilian Leopord.

Wiki ya unyonyeshaji inakwenda  na kaulimbiu isemayo  thamini unyonyeshaji weka mazingira wezeshi kwa mama na watoto kupitia ligi ya mpira.

Na Anwary Shaban.

Takwimu za miaka 30 iliyopita zinaonesha unyonyeshaji wa mama kwa mtoto zilikuwa chini ukilinganisha na kwa mwaka 2025 ambapo asilimia zimeongezaka na kufika 66% kwa watoto wanao nyonya maziwa ya mama pekee.

Hayo yamebainishwa na Bi Neema Joshua ambaye ni mkurugenzi Msaidizi wa huduma za lishe kutoka wizara ya afya katika viwanja vya St. John Dodoma ikiwa ni shughuli zinazofanyika kutoa elimu kwa jamii ta wiki ya unyonyeshaji inayo kwenda  na kaulimbiu isemayo  thamini unyonyeshaji weka mazingira wezeshi kwa mama na watoto kupitia ligi ya mpira.

Aidha Bi Neema ameeleza kuwa, ni muhimu mtoto kupatiwa maziwa ya mama pindi anapozaliwa kwani maziwa hayo yana vrutubisho vyote muhimu kwa mtoto.

Picha ni Afisa lishe jiji la Dodoma Bi. Semieva Juma akiongea katika wiki ya unyonyeshaji.Picha na Lilian Leopord.

Kwa upande wake eliet rumanyika ambaye ni Afisa lishe na mratibu lishe mama kutoka Wizara ya Afya ameeleza bado wataendelea kutoa elimu ya umuhimu wa maziwa ya mama hata baada ya maonesho kutokana na baadhi ya jamii kuwa na uelewa mdogo juu ya suala hilo.

Sanjari na hayo baadhi wa wazazi wameelza elimu waliyo patiwa katika madhimisho hayo ya unyonyesha ambapo wamesema elimu hiyo inakwenda kuwa saidia na jamii kwa ujumla.

Habari kamili