Unyanyapaa sababu kubwa waraibu kurudia matumizi ya dawa za kulevya
24 June 2026, 13:48

Serikali imekuwa ikisisitiza kuwa hakuna mwanafunzi anayepaswa kufukuzwa, kuzuiwa kufanya mtihani au kunyimwa huduma za msingi kwa sababu ya kutotoa mchango wa hiari.
Na Elizabeth Mwailunga.
Imeelezwa kuwa miongoni mwa sababu za baadhi ya waraibu wa dawa za kulevya kurejea katika uraibu baada ya kutoka soba house kunyanyapaliwa katika jamii na kutoshirikishwa katika shughuli za kijamii na kiuchumi.
Akizungumza na Taswira ya Habari,Mratibu wa kanda ya kati wa mtandao wa wamiliki wa soba houses Tanzania na mkurugenzi wa Dodoma soba house Elija Mwanga, baadhi ya watu waliotoka kwenye matibabu soba house hawawezeshwi kimitaji ya kuwawezesha kufanya shughuli za kujiingizia kipato ili kuendesha maisha yao hivyo kufanya utafutaji wao kuwa mgumu.
Aidha ameongeza kuwa katika ubunifu wa kimkakati Dodoma soba house wameanza kuhakikisha wanaweka msisitizo katika tiba kazi kama ufugaji wa kuku na ujuzi mwingine.
Ameeleza kuwa licha ya baadhi ya wazazi kuitikia vyema wito huo, bado kuna wazazi wachache ambao hawajashiriki kikamilifu katika michango hiyo, hali inayoweza kuathiri utekelezaji wa baadhi ya shughuli za maendeleo ya shule.
Mwanga ametoa wito kwa jamii kuacha kuwanyanyapaa watu waliopona uraibu wa dawa za kulevya na badala yake kuwapa ushirikiano na fursa za kujikwamua kiuchumi, ili kuwawezesha kuendelea na maisha mapya yenye tija.