Dodoma FM

Serikali yendelea kuhamasisha utunzaji wa mazingira

3 April 2023, 5:43 pm

Muonekano katika moja mitaa iliyopo hapa jijini Dodoma .Picha na Fred Cheti.

Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa mazingira imekuwa ikiiendeleea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Na Fred Cheti.

Serikali imekuwa ikihamasisha makundi mbalimbali katika jamii kushiriki katika utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kushiriki katika programu mbalimbali za utunzaji wa mazingira hayo ili kuhakikisha mazingira yanakua salama kwa kila kiumbe.

Moja kati ya makundi ambayo yanatajwa kuwa ni nguvukazi kubwa katika jamii  ni vijana ambapo kwa kuunga mkono juhudi hizo za serikali katika utunzaji wa mazingira Dodoma Tv imezungumza na baadhi ya vijana jijini hapa ili kujua nafasi ya kijana katika jambo hilo la utunzaji wa Mazingira.

Sauti za vijana
Muonekano katika moja mitaa iliyopo hapa jijini Dodoma .Picha na Fred Cheti.

Aidha vijana hao wametoa wito kwa vijana wenzao kujitokeza na kushiriki katika programu za utunzaji wa mazingira zinazoandaliwa na serikali pamoja na wadau wengine wa Mazingira

Sauti za Vijana.