Dodoma FM

Wakulima Wagomea mbolea ya Ruzuku

31 October 2023, 11:49 am

Picha ni Mkulima katika kijiji cha Chinangali 2 akiongea na Dodoma Tv kuhusu mbolea hiyo. Picha na Mindi Joseph.

Katika msimu wa kilimo wa mwaka 2021/2022, wakulima walinunua mbolea za kukuzia kama UREA kwa Sh110,000 kutoka Sh50,000 msimu wa 2020/21, huku mbolea nyingine za kupandia kama DAP ikinunuliwa kwa Sh120,000 kutoka Sh60,000.

Na Mindi Joseph.

Baadhi ya wakulima wa kijiji cha Chinangali 2 Mkoani Dodoma wamegoma Kujisajili kuchukua mbolea za ruzuku zinazotolewa na Serikali kutokana na kile wanachodai zinaua Mashamba yao.

Hayo yamebainika baada ya Dodoma Tv kufika eneo hilo na kuzungumza na wakulima hao kwa Nyakati tofauti kuhusu mwamko wao katika kujisajili na uchukuaji wa mbolea ya Ruzuku .

Wakulima hao wamesema hawana  imani na mbolea hiyo kama ilivyo ya samadi hali ambayo inasababisha  ugumu wa kujisajili ili kupata mbolea za ruzuku.

Sauti za Baadhi ya wakulima.

Afisa kilimo kijiji cha chinangali 2 Bi ,Asha Sume amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa wakulima juu ya mbolea hiyo ambapo juhudi hizo hazijazaa matunda ya kutosha katika kubadilisha fikra za wakulima za kujenga imani na mbolea hiyo.

Sauti ya Bi ,Asha Sume.
Picha ni Afisa kilimo kijiji cha chinangali 2 Bi ,Asha Sume. Picha na Mindi Joseph

Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea nchini TFRA Hivi karibuni iliwataka  wakulima nchini kuendelea kutumia mbolea ya Ruzuku.

Sauti kutoka TFRA.

Kuanzia mwaka 2003/2004, Serikali imekuwa ikitoa ruzuku kwenye kilimo  kwa njia tofauti tofauti na Katika msimu wa mwaka 2022/2023 tani 650,000 za mbolea ziliagizwa kutoka nje ya nchi.