Dodoma FM

Muendelezo wa jamii ya kabila la wasandawe na tamaduni zao

28 May 2026, 17:50

Wasandawe hufundishwa uwindaji tangu wakiwa wadogo watoto wa kiume hufundishwa kulenga shabaha.Picha na Mtanda.

Karibu katika fahari ya Dodoma ambapo leo tunaangazia asili ya kabila la wasandawe katika Kijiji cha Farkwa wilayani Chemba.

Na Yussuph Hassan.

Jamil hizi ambazo ni za kale zaidi na zinachukuliwa kuwa wakazi wa mwanzo kabisa wa jamil za asili ya Tanzania ziliishi kwa kuwinda wanyama wa porini kama swala, digidigi na wanyama wengine wadogo.

Pia, zilifanya shughuli ya kurina asali na kukusanya vyakula kutokana na mazao ya misitu, kama matunda, mizizi, mayai ya ndege wa porini na mizoga.