Dodoma FM

Watu wenye ulemavu waitaka jamii kuacha unyanyapaa

7 December 2021, 9:40 am

Na; Mariam Matundu.

Watu wenye ulemavu wameitaka jamii kuacha dhana potofu ya unyanyapaa na kuwaona ni watu wasioweza kujieleza pale wanapofika katika maeneo kutoa huduma mbalimbali .

Rajabu Mpilipili ni mkurugenzi wa taasisi ya Youth with disabilities organization na joyce wamesema mara nyingi wanapokwenda maeneo tofauti kupata huduma wakiwa na wasaidizi wao watoa huduma huzungumza na waliowasindikiza badala ya kuzumza na mtu mwenye ulemavu mwenyewe .

Amesema suala hilo wao huchukulia kama unyanyapaa kwakuwa wao wanahaki ya kusikilizwa na kujieleza kama watu wasio na ulemavu.

Nae Hassan Mikazi mwenyekiti wa chama cha wenye ualbino mkoa wa Morogoro amesema pia mtu yoyote anaewezesha mtu mwenye ulemavu kufikia au kupata huduma Fulani huchukuliwa kama ni msaada jambo ambalo si sahihi .

Akizungumzia suala la takwimu kwa watu wenye ulemavu mkurugenzi wa lukiza autism foundation Hilda Nkabe ameiomba serikali kupitia sense ya mwaka 2022 kuzingatia suala la wenye ulemavu ili kupata takwimu sahihi kutoka katika makundi yote ya watu wenyeulemavu.

Akijibia changamoto hizo kwa niaba ya mkurugenzi kutoka ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu , Afisa ustawi wa jamii Joyce Maongezi amesema ili kuendana na wakati na kutatua changamoto hizo serikali imeanza kupokea maoni kutoka kwa wadau yatakayo saidia kuboresha sera mbalimbali zinahusu kundi hilo.

Internews Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali kujadili ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika Nyanja mbalimbali na kutafuta suluhu ya changamoto zinazowakabili.