Dodoma FM

Diwani Nzuguni atakiwa kushughulikia changamoto yamigogoro ya  viwanja

8 May 2023, 4:27 pm

Diwani wa kata ya Nzuguni akiwa na wananchi wa kata hiyo wakati wa kusikiliza kero za viwanja. Picha na Mindi Joseph.

Mradi wa Visima vya Maji Nzuguni utaandika historia kwa wananchi kutokana na eneo hilo Tangu uhuru halijawahi kuwa na chanzo cha maji safi na salama.

Na Mindi Joseph.

Diwani wa kata ya Nzuguni Aloyce Luhega ameomba kushughulikiwa changamoto ya Migogoro ya viwanja kwa wananchi wanaopaswa kupisha Mradi wa Visima vya Maji Nzuguni.

Mh Aloyce amesema hayo wakati wa Usikilizwaji wa changamoto hizo ukitarajiwa kufanyika leo jumatatu na kesho jumanne kabla ya Uthamini kuanza siku ya Jumatano.

Viwanja hivyo 50 vinapaswa kupatiwa ufumbuzi kama anavyozungumza Diwani hiyo.

Sauti ya Diwani.
Usikilizwaji wa changamoto hizo unatarajiwa kufanyika leo jumatatu na kesho jumanne kabla ya Uthamini kuanza. Picha na Mindi Joseph.

Ameongeza kuwa viongozi wanapaswa kuhakikisha wananchi wanaopisha mradi huo wanapatiwa fedha zao.

Sauti ya Diwani.