Dodoma FM

Bodi mpya yatakiwa kusimamia kanuni, taratibu

28 July 2023, 2:41 pm

Waziri  wa  Viwanda na Biashara , Dkt Ashatu Kijaji akizungumza wakati akizindua Bodi ya sita ya ushauri. Picha na Selemani Kodima.

Pia amesema wana jukumu la kuishauri wizara kujua ni namna gani Wakala wa Vipimo iboreshe utendaji kazi wake.

Na Seleman Kodima.

Waziri wa Viwanda na Bashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji  amewataka wajumbe  wapya wa bodi ya sita ya ushauri ya Wakala wa Vipimo nchini kusimamia sheria, kanuni na taratibu katika utekelezaji wa majukumu yao mapya.

Waziri  Kijaji ametoa agizo hilo wakati akizindua bodi ya sita ya ushauri  Wakala wa Vipimo katika  hafla iliyofanyiwa ukumbi wa Mkandarasi jijini Dodoma.

Dkt Kijaji ameitaka bodi hiyo kufanya kazi kwa weledi na iwapo watakwama  basi watoe taarifa mapema.

Sauti ya Waziri wa Viwanda na Bashara .
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Bi Stella Kahwa akizungumza katika mkutano huo. Picha na Seleman Kodima.

Aidha Dkt Kijaji ameitaka bodi hiyo kuhakikisha watanzania wanaifahamu vyema wakala wa vipimo kupitia bidhaa ambazo zina vipimo sahihi .

Sauti ya Waziri wa Viwanda na Bashara .

Akitoa neno la shukrani, mwenyekiti wa bodi ya sita ya ushauri ya wakala wa Vipimo ambaye ni Afisa Mtendaji wa mkuu wa Wakala wa Vipimo Bi Stella Kahwa amemuhakikishia waziri kuwa kupitia ushirikiano wao na menejimenti  watahakikisha wanazitatua changamoto zote zinazolalamikiwa na wananchi

Sauti ya Afisa Mtendaji wa mkuu wa Wakala wa Vipimo.