Dodoma FM

Diwani Nkonko aahidi kuwasaidia vijana kupatiwa mkopo na halmashauri

29 April 2021, 6:00 am

Na; Seleman Kodima.

Diwani wa kata ya Nkonko wilayani Manyoni Ezekiel Samwel amesema ataendelea kupambana na kuhakikisha Vijana katika kata yake  wanachangamka na  Kupata mkopo unaotolewa Halmashauri kwa kundi la   wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili kujikwamua kiuchumi, kujiongezea kipato na kupunguza tatizo la ajira.

Akizungumza na Taswira ya Habari Diwani huyo amesema ataendelea kuhakikisha Vijana pamoja na watu wenye ulemavu wanapata mikopo ili kufanikisha wimbi la maendeleo katika kata hiyo.

Amesema kuwa wanawake ndio waliofaidika zaidi kupitia asilimia 10 za makundi hayo mpaka sasa tofauti na makundi mengine.

Kwa upande mwingine Bw Ezikiel amesema anatarajia kuanzisha mashindano ya vijana ikiwa ni sehemu ya kuwakutanisha Vijana ndani ya kata yake.

Nkonko ni Miongoni mwa kata chache Mkoani Singida ambazo zimebahatika kuwa na Diwani kijana ambaye amewahakikisha kundi la Vijana kuwa mstari wa mbele kuijenga Nkonko katika Nyanja za kiuchumi.

Na Selemani Kodima