Dodoma FM

Yafahamu madhara ya ugonjwa wa kipindupindu

18 January 2024, 8:56 am

Picha ni Afisa afya mkoani Dodoma Nelson Rumbeli akiendelea kutoa elimu juu ya ugonjwa wa kipindupindu. Picha na Yussuph Hassan.

Yafahamu madhara ya ugonjwa wa Kipindupindu endapo mtu atabainika kuwa na ugonjwa huo.

Na Yussuph Hassan.
Tukiwa katika muendelezo wa kupata elimu juu ya ugonjwa wa kipindupindu na leo tunafahamu madhara ya ugonjwa huo endapo mtu akibainika kuwa na kipindupindu.

Afisa afya mkoani Dodoma Nelson Rumbeli anaelezea madhara ya ugonjwa huo katika makundi mawili ikiwa ni kwa afya ya mtu na jamii pamoja na kiuchumi.