Dodoma FM

Serikali yachukua hatua mtoto aliyepotea Dar kurudishwa Mpwapwa

30 July 2026, 17:23

Mtoto huyo tayari yuko mikononi salama na utaratibu wa kumpelekea Mpwapwa unaendelea.Picha na mtandao.

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na vyombo vya dola kuhakikisha watoto wote wanaopotea wanapatikana na kurudishwa kwa wazazi wao.

Na Stephen Noel.

Serikali imesema imechukua hatua ya kumtafuta mtoto wa Mpwapwa aliepotea jijini Dar es Salaam na sasa imeshaanza utaratibu wa kumrudisha nyumbani.

Akizungumza na Dodoma FM, Kaimu Afisa Ustawi  Hamza Nyoni wa Jamii Wilaya ya Mpwapwa na Diwani wa Kata ya Lupeta, Sospeter Mdono wamesema mtoto huyo tayari yuko mikononi salama na utaratibu wa kumpelekea Mpwapwa unaendelea.

Viongozi hao wametumia fursa hiyo kuonya wazazi dhidi ya tabia ya kuwaruhusu watoto wadogo ambao walitakiwa wawe shule kwenda kufanya kazi za ndani mijini.

Sauti ya Noel.