Dodoma FM

Mahakama kuu divisheni ya kazi yaahidi kushirikiana na osha 

3 May 2023, 5:38 pm

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya  Kazi  Mhe. Yose  Mlyambina. Picha na Alfred Bulahya.

Dkt.  Mlyambina amemshukuru Mtendaji Mkuu wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA) kwa kuridhia mpango wa utoaji Elimu kwa Menejimenti  ya Mahakama Kuu Divisheni ya kazi.

Na Alfred Bulahya.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya  Kazi  Mhe. Yose  Mlyambina  amesema wataendelea kushirikiana na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ili kuhakikisha watumishi wanatekeleza majukumu yao katika hali ya usalama na afya bora.

Ameyasema  hayo  wakati wa  Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya  Usalama na Afya Mahali pa Kazi ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu  Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe, Prof. Joyce Ndalichako katika Uwanja wa Tumbaku Mkoani Morogoro.

Sauti ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya  Kazi 

Aidha Dkt Mlyambina Amesema  wameandaa mkakati wa kupokea elimu kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Usalama na Afya Mahali pa Kazi ambao  utahusisha Menejimenti ya Mahakama, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ili kujitathimi na kuzingatia sheria na kanuni za Usalama na Afya mahali pa kazi.