Dodoma FM

Athari za taka za plastiki kwa viumbe wa baharini na Afya za binadamu

16 February 2024, 4:46 pm

Plastiki hushikilia nafasi kubwa ya uchafu hatari zaidi na sugu baharini, ikikadiria asilimia 85 ya taka za baharini.Picha na HUDEFO.

Inaonyesha kwamba ingawa tuna maarifa, tunahitaji kujitolea kwa hatua za dharura ili kukabiliana na changamoto hizi zinazoongezeka kila siku katika mazingira.

Na Mariam Kasawa.

Uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya bahari unatajwa kuwa na athari kwa viumbe hai waishio chini ya maji kutokana na baadhi ya taka ikiwemo plastiki kuwa na madhara ya moja kwa moja kwa viumbe hao.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukizitaka nchi wanachama kuhakikisha wanadhibiti taka hizo katika mataifa yao ili kuokoa Maisha ya viumbe hai waishio chini ya maji pamoja na mfumo wa Ikolojia.

Tathmini hii inaangazia kiwango na madhara ya uchafu wa baharini na uchafuzi wa plastiki na kuchanganua masuluhisho na juhudi zilizopo.

Tathmini hii inaonyesha kuwa hatari kutoka kwa takataka za baharini na uchafuzi wa plastiki zinaongezeka katika mifumo yote ya ekolojia kuanzia kwa chanzo hadi kwa bahari.

Hii ni tathmini inayozungumzia kwa kina kuhusu utafiti wa sasa (na mapungufu ya maarifa) kuhusiana na athari za moja kwa moja kwa viumbe vya baharini, hatari kwa mifumo ya ekolojia na afya ya binadamu, na gharama kwa jamii na kwa uchumi.

Kwa ujumla, tathmini, ambayo inakusudiwa kuwezesha hatua zinazozingatia utafiti katika ngazi zote, inasisitiza umuhimu wa hatua za dharura kote ulimwenguni.