Dodoma FM

Milioni 255 zatengwa kumaliza tatizo la maji Mazae

4 February 2021, 12:31 pm

Na,Mindi Joseph,

Dodoma.

Wakati Vijiji vya Idilo na Kisokwe Wilayani Mpwapwa vinakabiliwa na changamoto ya maji kwa muda mrefu Serikali kupitia mamlaka ya maji Vijijini Ruwasa imetenga Shilingi Milioni 255 ili kutatua adha hiyo kwa wananchi.
Taswira ya habari imefika katika Kijiji cha Kisokwe na kuzungumza na Diwani wa Kata ya Mazae Mwl.William Madanya, ambaye amesema mradi huo tayari umeshafanyiwa upembuzi yakinifu, na upo kwenye utekelezaji.

Wakati mradi huo ukiwa kwenye utekelezaji, baadhi ya wananchi katika Kata hiyo wamesema hadi sasa ni bomba moja tu linatoa maji Kijijini hapo hivyo wanatarajia kuongezewa idadi ya mabomba ili kukomesha uhaba wa maji .

Naye Mwenyeikiti wa Kijiji Cha Mazae Kata ya Mazae Steven Paul Makasi ,amesema kwa muda mrefu wananchi wanahangaika kupata huduma ya maji kwani wanatoka Vijiji vya jirani na kufuata maji Kijijini hapo.