Dodoma FM

Mvua yachangia miwa kupanda bei sokoni

18 January 2021, 1:52 pm

Na,Shani Nicholous,

Dodoma.

Changamoto ya usafirishaji wa miwa imetajwa kama moja ya sababu inayochangia zao hilo kupanda bei ukilinganisha na hapo awali.
Miwa husafirishwa kutoka Mkoa mmoja hadi mwingine na kwa Dodoma wafanyabiashara wengi wamekuwa wakizipata kwa wingi Mkoani Tanga.
Wakizungumza na Taswira ya habari wafanyabiashara wa miwa katika soko la Bonanza jijini hapa wamesema kupanda kwa bei kumetokana na hali ya hewa kwa kuwa mvua inanyesha maeneo mengi ya nchi hali inayosababisha ugumu wa usafiri.

Kupanda kwa bei hiyo kumewaathiri hata wafanyabiashara wadogo wadogo ambao wamekuwa wakiitumia miwa hiyo kukamua juisi huku wengine wakiuza kwa kuzikata vipande na kuvifunga kwenye mifuko midogo.