Dodoma FM

Wawili wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za kujeruhi

10 December 2020, 2:51 pm

Na Zakia Ndulute,

Dodoma.

Mkazi wa Dabalo Wilaya ya Chamwino Bw.Msafiri Samson (38) na Samwel Msafiri (33) leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Dodoma kwa shitaka la kujeruhi kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Wakisomewa shitaka lao mbele ya Hakimu Mkazi wilaya ya Dodoma LILIAN TUNGARAJA na Mwendesha mashitaka ambaye ni wakili wa Serikali NEEMA TAJI amedai kuwa mnamo Oktoba 13 mwaka huu katika Kijiji cha Dabalo wilaya ya chamwino washitakiwa wote wawili walimshambulia MICHAEL PETRO kwa kumkata na kisu kwenye paji lake la uso na kumsababishia majeraha mwilini.
Hata hivyo Washitakiwa wote wamekana kutenda kosa hilo.
Naye wakili wa serikali NEEMA TAJI amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kumuomba Hakimu kuizuia dhamana ya shitaka hilo mpaka pale watakapopata taarifa sahihi za maendeleo ya majeruhi.
Kwa upande wake Hakimu TUNGARAJA amelipokea Ombi la wakili na kuamuru washitakiwa wapelekwe mahabusu mpaka pale Mahakama itakaporidhia hali ya mgonjwa kuwa nzuri.
Washitakiwa wamepelekwa rumande na shauri lao litatajwa tena Disemba 22 mwaka huu ikiwa ni pamoja na kusomewa masharti ya vigezo vya dhamana.