Dodoma FM

Chupa zenye haja ndogo zatupwa hovyo mitaani

5 February 2021, 4:19 pm

Na,Yusuph Hans,

Dodoma.

Wakazi wa Maeneo mbalimbali Mkoani Dodoma wamelalamikia tabia ya baadhi ya madereva wa daladala kujisaidia haja ndogo kwenye chupa za vinywaji na kuzitupa hovyo Mitaani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Taswira ya Habari baadhi ya wakazi hao wamesema, tabia hiyo imekuwepo kwa muda mrefu hali inayohatarisha afya zao

Nao baadhi ya madereva wamekiri kuwepo kwa tabia hiyo kwa baadhi yao ambao hufanya kwa sababu zao binafsi, na miongoni mwao ni wale wanaolala kwenye magari pamoja na malori ya Mikoani.

Akizungumzia suala hilo afisa afya wa jiji la Dodoma Bw.Abdallah Mahia amesema kumekuwepo na changamoto ya ushirikiano kwa wananchi katika kulinda mazingira pamoja na uhaba wa askari ambapo hizo ni miongoni mwa sababu za kuendelea kuwepo kwa vitendo hivyo.