Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuzingatia lishe bora

18 September 2023, 2:29 pm

Mtaalam wa lishe kutoka Taasisi ya  Agriculture Nutrition and Empowerment [ANUE] Bw. Mengo Chikombe akizungumza na Dodoma Tv. Picha na Diana Masaee.

Mara kadhaa Wizara ya Afya pamoja na taasisi mbalimbali za afya nchini zimekuwa zikitoa ushauri kwa  jamii kuzingatia ulaji wa lishe bora lengo ikiwa ni kuimarisha afya na kinga ya mwili.

Na Diana Massae.

Jamii  imetakiwa kuzingatia ulaji wa vyakula vyenye lishe bora hususani kwa watu wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwani husaidia kuimarisha afya ya mwili na huongeza siku za kuishi.

Ushauri huo umetolewa na mtaalam wa lishe kutoka taasisi ya  Agriculture Nutrition and Empowerment [ANUE] Bw. Mengo Chikombe Wakati akizungumza na Dodoma Tv ambapo amesema ni vyema kwa watu kuzingatia  ulaji wa mbogamboga na matunda ili  kuimarisha kinga ya mwili.

Sauti ya Bw. Mengo Chikombe.

Katika hatua nyingine  amesema  wanaendelea kushirikiana na serikali ikiwemo Wizara ya Afya kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya ulaji wa lishe bora.

Sauti ya Bw. Mengo Chikombe.
Picha ni aina mbalimbali za vyakula vyenye kujenga mwili. Picha na Mkulima mbunifu.

Dodoma Tv imekutana na baadhi ya wakazi wa Jiji la Dodoma ambapo wamesema hawana elimu juu ya kuzingatia ulaji wa lishe bora hivyo kutoa ushauri kwa waatalamu wa lishe Jijini Dodoma kutoa elimu kwa jamii juu ya suala hilo.

Sauti za baadhi ya Wananchi.