Dodoma FM

Baba, mama lishe watakiwa kuzingatia usafi

10 August 2023, 2:28 pm

upo umuhimu wa wafanyabishara hao kutumia mavazi maalumu kwani yanaashiria kuwa wanazingatia swala la usafi binafsi. Picha na Mariam Msagati.

Watoaji wa huduma ya vyakula katika maeneo mbalimbali ikiwamo migahawa na hotel wanashauriwa kuwa katika hali ya usafi ikiwemo uvaaji wa mavazi nadhifu ili kulinda afya ya walaji.

Na Mariam Msagati.

Usafi binafsi kwa wafanyabishara wanaojihusisha na biashara ya kuuza chakula maarufu kama Baba lishe na mama lishe umetajwa kama moja ya mambo ya msingi ya kuzingatia ili kufanya biashara hiyo katika hali ya mvuto na afya bora.

Dodoma tv imewatembelea baadhi ya mama lishe katika eneo la majengo jijini Dodoma na hapa wanaeleza umuhimu wa kutumia mavazi maalum kwa ajili ya kujisitiri katika biashara hiyo.

Sauti za baadhi ya mama lishe.

Baadhi ya wateja wanasema kuwa upo umuhimu wa wafanyabishara hao kutumia mavazi maalumu kwani yanaashiria kuwa wanazingatia swala la usafi binafsi, usafi wa mazingira yanayo wazunguka pamoja na kuvutia wateja.

Sauti za baadhi ya wateja.
Picha ikionesha eneo wanalo kaa wateja wa chakula kwaajili ya kupata chakula. Picha na Mariam Msagati.

Bi Rhoda Boi ni mwenyekiti wa kamati ya afya na mazingira katika soko kuu la majengo Jijini Dodoma anaeleza umuhimu wa wafanyabishara wa vyakula pamoja na wauzaji wa nyama kuvaa mavazi meupe na kofia ili kulinda afya za walaji.

Sauti ya Mwenyekiti wa kamati ya Afya na mazingira soko kuu Majengo.