Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuendelea kupiga vita vitendo vya ukatili

24 April 2024, 6:32 pm

Picha ni tamasha la kupinga vitendo vya ukatili lililofanyika Wilayani Mpwapwa.Picha na Steven Noel.

Afisa Ustawi wa jamii wanazungumzia vyanzo vya ukatili na jinsi ya kuepukana na vitendo hivyo.

Na Steven Noel.
Jamii imeshauriwa kuendelea kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa makundi yote Ili kuweza kuwa na Taifa lenye amani na maendeleo.

Hayo yamesemwa kwenye tamasha la kuelimisha Jamii dhidi ya kupinga vitendo vya ukatili liliondaliwa na wadau wa huduma za mtoto wilayani Mpwapwa.

Zakaria Kiondo ni afisa maendeleo ya jamii na Ruth Mudamo ni Afisa Ustawi wa jamii wanazungumzia vyanzo vya ukatili na jinsi ya kuondokana nao.