

6 May 2025, 5:29 pm
Hata hivyo serikali ilishatangaza ujauzito isiwe sababu ya mwanafunzi kuacha masomo hivyo kuwaruhusu wanafunzi waliokatiza masomo yao kwa sababu hizo kurejea shuleni.
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa umbali wa kilomita kumi kuifikia sekondari kwa wanafunzi wa kijiji cha Muungano imekuwa sababu ya wasichana wengi kukatiza masomo yao kwa changamoto za kubeba ujauzito.
Hayo yameelezwa na wanazengo wa wa kijiji hicho ambao tayari wameenza kuchukua hatua za ujenzi wa sekondari ndani ya kijiji chao.
Wamesema kuwa umbali wa kufika kijiji cha Ilolo ilipo shule hiyo imekuwa ikipelekea vishawishi kwa watoto wa kike na kukatisha ndoto zao kwa kuambulia kubeba ujazito.
Aidha pamoja na adha hiyo bado umbali huo umekuwa ukipelekea kuchelewa vipindi vya darasani hususani vipindi vya asubuhi
Mwenyekiti wa kijiji hicho Ndg.Matonya Mtukamsihi amekiri changamoto hiyo imepelekea watoto wengi kukimbilia mjini kufanya kazi za ndani
Huku wengine wakipoteza matumaaini baada ya kupata ujauzito hali inayotokana na kukosekana kwa uangalizi wa wazazi wao