

17 April 2025, 6:11 pm
kwasasa wapo katika changamoto ya shule kulemewa hivyo majengo ya shule mpya nahitaji milioni 36 za ujenzi wa vyoo ndipo ianze kutumika Kwa kupunguza mjazano wa shule mama.
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa matumizi mazuri ya rasilimali ni pamoja na rasilimali hizo kutumika kwa manufaa ya wananchi wa eneo hilo.
Hayo yamezungumzwa na Diwani wa Kata ya Ihumwa Ndg.Edwadi Magawa Kwa kuwasihi wananchi waliopo katika mradi SACCOS ambao umelenga kilimo Cha umwagiliaji katika Korongo la ihumwa
Magawa amesema kuwa licha ya uwepo wa taasisi hiyo lakini umekosekana ulinzi madhubuti wa kulinda mchanga na kupelekea biashara binafsi Kwa wachache.
Na linapo fika suala la Serikali ya Mtaa kutaka kutumia rasilimali hiyo ndipo taasisi hiyo inaibuka na kuzuia Kwa madai ya shughuli za kilimo.
Magawa amesema kuwa kwasasa wapo katika changamoto ya shule kulemewa hivyo majengo ya shule mpya nahitaji milioni 36 za ujenzi wa vyoo ndipo ianze kutumika Kwa kupunguza mjazano wa shule mama
Aidha malengo ya Serikali ya mtaa ilikuwa ni kutumia sehemu ya mchanga ulipo Korongonili kufanikisha ujenzi wa matundu ya vyoo yasiyo pungua ishirini.
Josia Njilimuyi Mwenyekiti wa jumuiya ya SACCOS amesema ni vyema Serikali kutafuta njia sahihi ya ujenzi wa matundu ya vyoo ikiwa ni pamoja na kufanya makusanyo ya nyumba Kwa nyumba.